Ungana nasi kuitaka serikali kwa kupitia Bunge kutunga sheria, kupinga ukatili wa kijinsia

  • by: Neema R
  • recipient: Mpendwa Mtanzania
Mpendwa Mtanzania,

Ukatili wa kijinsia ni janga la kitaifa na hatua madhubuti zisipochukuliwa basi tunu kubwa za taifa letu ikiwemo utu na heshima zitakuwa hatatani. Ukatili wa kingono, vipigo, mila kandamizi kama ndoa za utotoni na Ukeketaji, ukatili wa majumbani, ukatili wa kiuchumi, udhalilishaji wa kimwili vyote hivi ni baadhi tu ya aina za ukatili ambao umeendelea kukiuka misingi ya haki za binadamu na haki za wanawake hapa nchini.

Je wajua Ndoa za Utotoni ni 36% hapa nchini? Na kwamba kati ya watoto wa kike 5 wawili huozeshwa kabla ya kutimiza miaka 18?
Je wajua Ukeketaji ni 10% hapa nchini?
Je wajua wasichana wanaopata mimba mashuleni ni 26%?
Je wajua vikongwe takribani 124 waliuwawa kati ya Julai 2015 and Machi 2016 na kufikisha idadi ya vikongwe 1,423 waliouwawa kuanzia 2013 hadi 2016?
Je wajua katika jiji la Dar es Salaam kwa wastani wanawake au wasichana 3 walibakwa kila siku kwa mwaka 2016?
Je wajua kesi 5,802 za ubakaji ziliripotiwa mwaka 2015 na hii ni sawa na wastani wa wanawake 483 walibakwa kila mwezi, ikimaanisha kuwa angalau wanawake au wasichana 16 walikuwa wanabakwa kila siku hapa nchini?
Je wajua kwa wastani matukio 1400 ya Ukatili kwa wanawake yalitokea kila mwezi kwa mwaka 2015?

Aibu Aibu Aibu! Matukio haya na mengine mengi ni aibu kwa taifa na ni ukiukwaji wa haki za binadamu na haki za wanawake.

Hivyo basi kwa kutambua misingi hii tunakuomba ndugu Mtanzania uungane nasi kuitaka serikali kwa kupitia Bunge letu kutunga sheria ya kupinga ukatili wa kijinsia ambayo itawezesha kudhibiti janga hili.

Ndugu Mtanzania kumbuka kwamba Tanzania imeridhia mikataba mingi ya kikanda na ya kimataifa inayopinga ubaguzi na ukatili dhidi ya wanawake na inayotaka uwepo wa sheria zinazojenga misingi ya haki na usawa na kuweka ulinzi kwa wanawake.

Tafadhali tumia dakika moja tu kuweka sahihi yako ya kutaka kuwepo kwa sheria hii ya kupinga ukatili wa kijinsia.

Pamoja tunaweza kumlinda mwanamke wa Tanzania dhidi ya Ukatili wa Kijinsia.

Weka sahihi yako Sasa! Thubutu Kuleta Mabadiliko!
Sign Petition
Sign Petition
You have JavaScript disabled. Without it, our site might not function properly.

Privacy Policy

By signing, you accept Care2's Terms of Service.
You can unsub at any time here.

Having problems signing this? Let us know.